Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Friday, September 20, 2013

Marekani yataka UN iichukulie hatua Syria

WASHINGTON, Marekani
SERIKALI ya Marekani imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa (UN), kuja na azimio la kuichukulia hatua serikali ya Syria kwa kosa lake la kutumia silaha za kemikali.
Marekani imetoa wito huo kwa UN, Jana ikiutaka umoja huo kuichukulia hatua Syria kwenye mkutano uliopangwa kufanyika wiki ijayo jijini New York.
Akizungumzia hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amesema kuwa mgogoro wa Syria umefikia katika hatua ya mvutano na kinachotakiwa ni UN kupitia baraza lake la usalama kutekeleza kazi zake kwa vitendo.
Kerry alisema kuwa muda wa malumbano umekwisha na kinachotakiwa ni kuhakikisha silaha za kemikali zinaharibiwa huko Syria kwa kuwea tafsiri ya ripoti ya UN inaonyesha kuwa serikali hiyo inahusika na matumizi ya silaha hizo.
Kiongozi huyo amesema UN inawajibika kujiandaa kuchukua hatua kuhusiana na silaha hizo za kemikali ambazo zimesababisha mauaji ya raia wasiokuwa na hatia.
Wakati huohuo Rais Iran Hassan Rowhani amesema kuwa yuko tayari kuratibu mazungumzo ya amani kati ya Serikali ya Syria na upinzani ili kumaliza mgogoro huo ambao unaendelea kuiyumbisha Jumuiya ya kimataifa.
Rais Iran Hassan Rowhan amesema kuwa nchi yake iko tayari kusuluhisha pande hizo ili amani ipatikane nchini Syria kama njia ya kutekeleza sera ya Iran ya kujenga badala ya kubomoa.

Serikali ya Syria bado inashikilia msimamo wake kuwa haikutumia silaha za kemikali licha ya kukubali kuziharibu ndani ya mwaka mmoja, silaha ambazo inazimiliki.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text