Changanyikeni
waandamana hadi Dawasco
DIWANI wa
kata ya Makongo, Deusdedit Mtiro ameungana na wakazi wa eneo la Changanyikeni
na kwenda Mamlaka ya Majisafi na
Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), kutoa malalamiko yao ya kukosa maji kwa muda wa
miaka saba.
Malalamiko hayo
waliyepeleka jana katika ofisi za Dawasco Kimara, jijini Dar es Salaam kwenye
ofisi za Meneja wa ofisi hiyo, Rukia Bachu.
Diwani Mtiro
alianza kumueleza malalamiko yao Meneja huyo, Rukia kuwa Wananchi wa eneo la
Changanyikeni wamekuwa katika tabu ya kukosa maji tangu mwaka 2006 hadi sasa.
Diwani Mtiro
alisema “Nakumbuka mwaka 1989 tulikuwa tukipata maji vizuri, kupitia bomba
ambalo tulikuwa tumelinunua kwa nguvu za wananchi, lakini mwaka 2006 mambo
yalibadilika baada ya Dawasco kufunga mabomba ya Mradi wa Wachina, ndipo
tulikosa maji mpaka leo,”.
Naye Mkazi
wa eneo hilo Erick Mchata alisema kuwa wamekuwa wakifika mara kwa mara katika
ofisi hizo ikiwamo Makao Makuu Dawasco lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika
kwa ajili ya kutatua tatizo lao.
Mkazi mwingine,
Mzee Kamba anasema anashangaa pamoja na kukosa maji kwa muda lakini amepelekewa
bili ikionesha anadaiwa sh 1,000,000.
Kwa upande
wa Mengyason Masawe alisema kuwa anaumia kuona maeneo yaliyo juu yao wanapata
maji lakini wao wakikosa hata kwa siku moja kwa wiki.
Akizungumzia
malalamiko hayo Meneja wa Dawasco wa Kimara, Rukia Bachu alikiri kuwepo kwa
tatizo la kukosekana kwa maji katika eneo hilo kwa muda mrefu.
Akielezea
sababu ya kuwepo kwa tatizo hilo anasema kuwa “Tatizo kubwa eneo hilo limekuwa
likichangiwa na baadhi ya watu kumiliki matenki yenye ujazo mkubwa kiasi cha
kusababisha wengine kukosa, hivyo ninawaomba mtusaidie kuwafichua wanaofanya
mchezo huo ili kuwezesha kutatua tatizo hilo,” alisema Rukia.
Meneja Rukia
aliwaahidi kulishughulikia tatizo hilo na kuwawezesha wananchi hao kupata maji
siku ya jumamosi ambako atamtuma mhandisi kwenda kuwaunganishia maji hayo ikiwa
ni pamoja na kuwezesha kuwafichua wale wanaotumia matenki makubwa.
0 comments:
Post a Comment