Garden Fc yang'ara Mama Kevin Cup
KOMBE la Mama
Kevin limefikia tamati mwishoni mwa wiki kwa timu ya Garden FC ya Mtoni kwa
Azizi Ali kutwaa ubingwa baada ya kuichapa timu ya Jiulize FC kutoka Tandika
kwa mabao 2-0.
Katika
fainali hizo zilizopigwa kwenye uwanja wa Sifa Mtoni, mtaa wa Sabasaba jijini
Dar es salaam timu ya Galden FC iliyoibuka mshindi walikabidhiwa zawadi zao na Katibu
wa Chadema Mkoa wa Temeke, Aloyce Waryoba.
Zawadi
walizopewa ni kombe lenye thamani ya shilingi 550000, jezi zenye thamani ya 250,000, mpira wenye thamani ya shilingi 40,000 na mbuzi
mwenye thamani ya shilingi 100,000 sambamba na fedha taslimu shilingi 100,000.
Wakati
mshindi wa pili Jiulize FC waliozawadiwa
jezi zenye jezi zenye thamani ya 250,000,
mpira wenye thamani ya shilingi 40,000 na mbuzi mwenye thamani ya shilingi
100,000 sambamba na fedha taslimu shilingi 50,000.
Kwa upande
wa mfungaji bora aliyefunga mabao saba, Juma Bahanuzi kutoka Jiulize FC
aliyezawadiwa ngao ya kiatu cha dhahabu chenye thamani ya shilingi 100,000
sambamba na fedha shilingi 100,000.
Shindano
hilo la soka lililodhaminiwa na Mwenyekiti wa Kata ya Chang’ombe kupitia chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edith Bunjoro ‘maarufu kama mama Kelvin’
lililozinduliwa Julai 14 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha ualimu (Duce) na
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Katika
uzinduzi huo Mnyika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA) Taifa, alisema
katika ilani ya uchaguzi ya CHADEMA 2010, ilikuwa ni suala walilokuwa
wamelipatia kipaumbele.
Mashindano
hayo yalishirikisha timu kutoka kata zote za Manispaa ya Temeke ambazo ni Senet
FC, Ubaya FC, Depo FC, Umoja FC, Scud,
Panama, Masofa FC, Home Boy, Pama, Texas, Wajivuni, Wadude, Maji maji, Miduza,
Jiulize na Dar United.
Katika
shindano jingine la kuvuta kamba lililoshirikisha makundi mawili yote kutoka
eneo la Mtoni washindi walikabidhiwa zawadi ya mbuzi mwenye thamani ya shilingi
100,000.
Pia kulikuwa
na shindani la kufukuza kuku lililokuwa limewashirikisha wanachama wa Baraza la
Wanawake Chadema wa kata ya Chang’ombe (BAWACHA) ambalo mshindi aliibuka kuwa
Bishala Dausi aliyejishindia kuku mwenye thamani ya shilingi 20,000.
Katika mashindano kama hayo ya kufukuza kuku
lililoshirikisha akina mama wote wa Mtoni bila kujali itikadi za chama, Amina
Saidi aliibuka kidedea kwa kujishindia kuku mwenye thamani ya shilingi 20,000.
0 comments:
Post a Comment