Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Wednesday, September 4, 2013

Putin: Harakati za kijeshi Syria ni Uvamizi

DAMASCUS, Syria
RAIS wa Urusi Vladimir Putin, ameionya Marekani na nchi za Magharibi kuhusu hatua za kijeshi wanazofikiria kuchukua dhidi ya Syria kuwa zitakuwa za kivamizi.
Alionya kuhusu kuchukua hatua zozote za kijeshi dhidi ya Syria  itakuwa ni uvamizi.
Kauli hiyo imekuja hivi karibuni baada ya Rais wa Marekani Barack Obama kutoa wito wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria baada ya kusema kuwa kuna uthibitisho kuwa rais Assad ametumia silaha za kemikali dhidi ya wananchi wake.
Lakini kwenye mahojiano na shirika la habari la Associated Press(AP), kabla ya mkutano wa wiki hii wa G-20 mjini St Petersburg, Putin alisema kuwa huenda akaunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa (UN), ikiwa kuna thibitisho kuwa silaha za kemikali zilitumiwa dhidi ya raia.
Putin alipuuza wasiwasi kuwa wanariadha au mashabiki wataadhibiwa ikiwa watatoa matamshi yatakayoonekana kuwa propaganda kuhusu mapenzi ya jinsia moja wakati wa michezo ya olimpiki itakayofanyika nchini humo.
Wakati huohuo, maseneta nchini Marekani wameridhia mswada wa azimio linalompa idhini Rais Barack Obama kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi ya Syria.
Pamoja na kuriudhia lakini mswada huo unatarajiwa kupigiwa kura wiki ijayo.
Awali Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry alifika mbele ya Baraza la Seneti ambapo alitoa onyo kwa maseneta wa Marekani kabla ya mdahalo wao kuhusu Syria unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo kwamba, hawapaswi kushindwa kutoa jibu la kile alichokitaja kuwa ni matumizi ya silaha za kemikali ambayo hayawezi kukanushwa yaliyofanywa na Rais Assad kwa watu wake mwenyewe.

Naye Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ikiwa itathibitishwa kwamba silaha za sumu ya kemikali zilitumiwa nchini Syria, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lazima liungane na kuchukua hatua.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text