Kaka ndani ya AC
Milan
MAKAMU wa rais wa klabu ya AC
Milan, Adriano Galliani amethibitisha klabu yake kumsainisha mchezaji Ricardo
Kaka anayekipiga Real Madrid.
Kaka anatarajiwa kurejea Milan,
ambako anaamini atafurahia maisha yake ya soka, baada ya kukaa Bernabeu kwa
muda wa miaka minne kwa dili la pauni milioni 56.
Mchezaji huyo mwenye miaka 31 amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili
mwishoni mwa wiki hii.
Kaka alikosa raha katika muda
wake wa uchezaji kutokana na kusombuliwa na majeruhi.
Lakini mchezaji huyo wa
kimataifa wa Brazil anaamini kiwango chake kitarudi kama zamani mara ya kwanza
alipokuwa San Siro.
Taarifa za Milan zimeeleza
kuwa: "usiku wa jana tumeboresha zaidi uhusiano wetu na klabu za Real
Madrid kwa kuwezesha kuturudishia mchezaji Ricardo Kaka.
0 comments:
Post a Comment