H&B Agerup Foundation: WLF imeutendea haki mradi
TAASISI ya
H&B Agerup Foundation ya nchini Marekani imeeleza kuridhishwa na utendaji
mzuri unaofanywa na Taasisi ya nchini ya World Lung Foundation (WLF), katika
mradi wake wa kuokoa vifo vya mama na mtoto.
Akizungumza
juzi, Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Taasisi ya H&B Agerup Foundation ambao
ni wafadhili wakuu wa mradi huo, Dk. Helen Agerup aliimwagia sifa WLF baada ya
kutoka katika ukaguzi wa mradi huo unaoendelea mkoani Kigoma.
Dk Agerup alisema
kuwa “Nikiwa Kigoma nikikagua vituo tisa vya afya ambavyo vimo katika mradi wa
WLF na nimeshuhudia wafanyakazi 26, waliopewa mafunzo ikiwamo na wananchi wa
eneo hilo”.
Anaongeza kuwa
akiwa katika mkoa huo alikutana wafanyakazi wa afya pamoja na viongozi wa
Serikali na kubaini kwamba tangu mradi huo ulipoingia wajawazito wamekuwa
wakihudhuria katika vituo vya afya ukilinganisha na hapo awali.
Alisema
kuwa kabla ya mradi huo wajawazito waliokuwa wakihudhuria katika vituo vya afya
kwa mwaka 2006 walikuwa 885, lakini baada ya kupata elimu kutoka WLF idadi hiyo
imeongezeka mara dufu kwa Januari 2012 hadi Agosti 2013 wameongezeka na kuwa
1528”.
Dk. Agerup
aliongeza kuwa katika kituo cha afya cha Ujiji kimeonesha mafanikio makubwa
kwani mwaka 2007 wanawake waliokuwa wakihudhuria kituo cha afya walikuwa ni
nane lakini mwaka jana walifikia 2,634.
Kutokana na
mafanikio hayo Dk. Agerup aliahidi kuendelea kukufadhiri vituo vya afya na
mradi kwa ujumla.
“Nawaahidi
kushirikiana nao kwa karibu sambamba na serikali ya Tanzania nia ikiwa kupata
matokeo chanya katika mradi huo wa afya ya mama na mtoto,” alisema Dk. Agerup.
Naye
Mkurugenzi wa Mradi wa WLF, Dk. Nguke Mwakatundu alisema kuwa Taasisi hiyo
imepanga kuongeza vituo vingine 10 vya afya katika miaka miwili ijayo ili
viungane na vya sasa ambavyo ni 10.
Akielezea
mafanikio ya mradi huo katika kuzuia vifo vya uzazi, Dk. Mwakatundu alisema
kuwa kwa sasa wamefanikiwa ukilinganisha na mwaka 2006 -2011 ambako idadi yao ilikuwa
31 lakini baada ya mradi huo imepungua na kufikia watu watatu kwa miaka miwili
ya 2012 -2013.
Dk. Mwakatundu
alitoa wito kwa Serikali na asasi nyingine kuendeleza mradi huo katika mikoa
mingine kama wao wanavyofanya kwa Kigoma.
0 comments:
Post a Comment