Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Wednesday, September 25, 2013



Waajiri watii sheria ya ajira kwa watu wenye ulemavu

WAAJIRI wameshindwa kutii sheria ya ajira ya mwaka 2010 inayowataka wale wenye wafanyakazi zaidi ya 20, wahakikishe asilimia tatu ya wafanyakazi wao wawe watu wenye ulemavu (WWU).
Hayo yamebainishwa jana, Dar es Salaam na Meneja Programu ya utetezi Fredrick Msigallah, wakati akiwasilisha mada yake kwenye uzinduzi wa ripoti za utafiti kuhusu Ajira kwa watu wenye ulemavu uliofanywa  kwa kushirikiana na  Taasisi ya kusaidia walemavu ya (CCBRT) na Radar Development.
Akiwasilisha mada hiyo, Msigallah alisema katika utafiti huo walizishirikisha sekta binafsi kutoka mikoa ya Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Morogoro na Tanga kwa kushirikiana na Chama Cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Fedha (TUICO), ukiwa umezihusisha jumla ya kampuni 72 zilizo na wafanyakazi 50.
Akiwasilisha alisema kuwa tathmini yao inaonesha idadi ya watu wenye ulemavu katika sehemu za kazi bado iko chini.
Akithibitisha hilo anasema kwamba katika Kampuni hizo zilizofanyiwa utafiti zinaonesha kati ya wafanyakazi 20,568 ni wafanyakazi 86 pekee ambao ni asilimia 0.4 ndiyo wenye ulemavu.
Anaongeza kuwa kati ya Kampuni hizo 72 zilizofanyiwa utafiti huo ni mbili pekee zilizofikisha zaidi ya asilimia tatu ya wafanyakazi wenye ulemavu na hivyo kukidhi matakwa ya sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 inayomtaka bayana kuwa kila mwajiri mwenye wafanyakazi zaidi ya 20 ni asilimia tatu ya wafanyakazi hao wawe wenye ulemavu.
Akielezea sababu inayochangia kutokea kwa tatizo hilo Msigallah alisema “Utafiti unaonesha kuwa waajiri wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu sheria hiyo na sera zinazosimamia masuala ya ajira kwa watu wenye ulemavu, kwani kati ya kampuni zilizofanyiwa utafiti ni asilimia 40 pekee viongozi wake walionesha kufahamu sheria na sera zinazohusu ajira kwa watu wenye ulemavu,”alisema Msigallah.
Akielezea utafiti walioufanya katika sekta ya elimu wakiwa wameshirikiana na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ukiwa umelenga walimu wa msingi sekondari na vyuo wa mikoa ya Dar es Salaam, Mara, Lindi, Mbeya, Singida na Tabora ambako walibaini kuwa kuna walimu 24,552 na wale waliokuwa na ulemavu walikuwa 519 ambao ni asilimia 2.1 pekee.
Msigallah aliongeza kuwa utafiti huo ulibaini kuwa walimu wenye ulemavu wanaopata nafasi za uongozi ni ndogo huku wengi wao wakiwa wanaume ambako wale wenye nafasi ya mwalimu mkuu walikuwa 519 na miongoni mwao asilimia 79 ni wanaume na asilimia 21 ni Wanawake.
Katika sekta ya Afya, anasema walifanya utafiti kwa kuwashirikisha Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii walibaini miongoni mwa wafanyakazi 738 ni 17 pekee ndio walikuwa wenye ulemavu na miongoni mwa hao ni asilimia 64.7 walikuwa wanaume na wanawake asilimia 35.3.
Naye Mkurugenzi wa Ajira wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ally Msaki, alikiri kuwepo kwa changamoto nyingi zinazochangiwa na historia ya kiimani na kitamaduni.
Msaki anasema changamoto nyingine ni namna ya kusimamia utekelezaji ambao hata hivyo hivi sasa serikaliu imeanza kwa kufanyika utafiti mkubwa kwa kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kujua mahitaji mbalimbali ikiwamo ajira kwa watu wenye ulemavu.
Alisema kuwa njia ya kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata ajira kwa kupitia sheria ya mwaka 2010 ni kufikiria kutoa motisha na elimu kwa waajiri.
“nitahakikisha nashirikiana na viongozi wenu katika kuhakikisha tunafanikiwa katika suala hilo la ajira,” alisema.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text