Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Saturday, September 21, 2013

Mabasi ya haraka yakalibia kuanza  

MAGARI 366 yanatarajiwa kutumika katika mradi wa wakala wa usafiri wa haraka jijini Dar es Salaam(DART).
Hayo yamebainishwa jana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa DART, Asteria Mlambo katika mkutano uliowashirikisha DART na wamiliki wa Daladala wa jiji la Dar es Salaam.
Astela akifafanua mpango kazi wa mabasi hayo, katika awamu ya kwanza ya mradi ambako alisema utatumia mabasi makubwa 145 na mengine madogo 221.
Alisema makubwa yatakuwa katika vituo vikubwa wakati madogo yatakuwa na kazi ya kuwatoa wasafiri katika maeneo ya pembezoni mwa mji na kuwapeleka katika vituo vya mabasi makubwa.
Aliwatoa hofu wasafiri watakaokuwa wanatolewa pembeni na magari hayo madogo kuwa hawatalipa nauli mara mbili.
Asteria alisema ili wamiliki wa daladala wafaidi umiliki wa mradi huo wanatakiwa kuanzisha kampuni mbili.
Alisema kuwa miongoni mwa Kampuni hizo iwapo itaamua kuungana na nyingine ya nje yenye uzoefu katika masuala ya usafiri kwa ajili ya kujipatia uzoefu huo haitazuiwa.
Akielezea faida za kuanzishwa kwa Kampuni hizo alisema zitawawezesha kupata mikataba ya umiliki wa mradi huo kwa kusimamia shughuli za ukatishaji wa Nauli ambazo zitakuwa katika mfumo wa kadi kama zile zitumikazo benki ikiwamo na umiliki wa mabasi katika mkatrabga utakaotumia miaka 12.
Alisema “tunahitaji umiliki wa miradi hiyo iende mikononi mwa wamiliki wa daladala ambao watapewa mabasi kwa kuchanganyiwa madogo na makubwa,”.
Faida nyingine alisema ni kutoa kipaumbele kwa wamiliki wote wa daladala zinazotumia barabara ya Morogoro kwa kuchangia mtaji wa mradi kwa njia ya hisa.
Kuhusu wasiwasi wa suala la mapato, Mlambo aliwaeleza wamiliki hao kuwa mazingira waliyotengeneza yatawawezesha kudhibiti mapato kwa kutumia tiketi za kadi mithiri ya zile zinazotimiwa na benki.
Aliongeza kuwa wataangalia malipo kulingana na kilomita ambazo gari itakuwa imekwenda hivyo kusaidia wakati gari linapokuwa halijafanya shughuli kutotozwa.
Kuhusu magari yaliyokuwa yakifanya shughuli zake katika barabara ambazo mradi huo unapita, daladala zao zitatakiwa kupelekwa kufanya kazi katika barabara za nje ya mji.
Alitaja njia kuu ambazo zitatumika katika mradi huo wa awamu ya kwanza ambao utatumia njia kuu za Kimara hadi Kariakoo, Ubungo hadi Feri, Morroco hadi Kariakoo na Morocco hadi Ubungo.
Naye Mkuu wa Mkoa, Said Meck Sadik alisema kuwa amefarijika na mradi huo kwa sababu utapunguza msongamano wa magari hivyo kusaidia watu kuwahi katika shughuli zao.
Meya wa jiji la Dar es Salaam Dk. Didas Masaburi amesema kuwa watahakikisha mradi huo unakuwa wa faida kwa kuepusha kutokea kama yale ya Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) na mabasi mengine ya usafirishaji wa mkoani.
Akizungumzia kuhusu magari hayo kama ni rafiki kwa walemavu alisema kuwa sehemu yake ya kupanda ina wasaidia pia watu wenye ulemavu.
Masaburi aliongeza kuwa katika mpango huo serikali haitakuwa na kazi ya kuhusika na biashara na badala yake kubaki katika kuangalia miundombinu pekee.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text