Mandela atoka hospitali,
arejea nyumbani
JOHANNESBURG, Afrika kusini
SERIKALI ya nchini Afrika
Kusini imesema kuwa rais wa zamani wa nchini humo, Nelson Mandela (95),
ametolewa hospitali leo alikokuwa akitibiwa mapafu tangu Juni.
Taarifa za kutolewa kwake
hospitali na kurejea nyumbani zilitolewa kwenye tovuti ya Rais wa nchi hiyo zikieleza
kuwa Mandela bado yu mahtuti na hali yake wakati mwingine inabadilika.
Lakini madaktari wake
wanaamini akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg atapata matibabu sawa na yale
ya hospitali.
Nyumba ya Mandela
imebadilishwa ili kumruhusu kupata matibabu ya mgonjwa mahtuti akiwa nyumbani.
Serikali imesema inamtakia
mema wakati akiendelea na matibabu.
0 comments:
Post a Comment