Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Monday, September 2, 2013

United kufunga dirisha dogo na Ozil?           

KLABU ya Manchester United imeungana na Arsenal katika kinyang’anyiro cha kumsainisha mchezaji wa Ujerumani anayekipiga Real Madrid, Mesut Ozil na leo ikiwa ndio mwisho mwisho wa usajili wa dirisha dogo.
Taarifa hizo zimetolewa na mtandao wa Sky Sports ukisema imekuwa ikitapatapa baada ya kupokea kipigo cha 1-0 dhidi ya Liverpool katika mechi iliyopigwa mwishoni mwa wiki hali iliyosababisha kocha David Moyes kupigana kufa na kupona ili kumpata Ozil.
Arsenal, nayo imeonesha nia ya kufanya kufuru katika kuhakikisha inamtwaa mchezaji huyo kwa usajili utakaofikia kiasi cha Euro milioni 42.5.
Kocha wa Arsene Wenger alibainisha mipango yake baada ya kumalizika kwa mechi yao ya jumapili waliyoibuka na ushindi wa kupata bao 1-0 dhidi ya klabu ya Tottenham.
Alisema "tuymepanga kufanya maajabu kwa mchezaji huyo katika saa 24 zijazo, ingawa ni uamuzi mgumu lakini wa kushtua."
Ozil (24), alisaini kukipiga Real akitokea Werder Bremen mwaka 2010 kwa dili la euro milioni 15 lakini amekuwa akipambana kutafuta kucheza kikosi cha kwanza.
Ingawa taarifa kutoka Hispania zinasema kuwa mchezaji Ozil hatakwenda kokote bali ataendelea kupigania namba chini ya kocha Carlo Ancelotti.

Kwa nyongeza Ancelotti aliyekuwa akifundisha Paris Saint-Germain anatarajia kuzungumzia suala la Ozil.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text