Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Wednesday, September 25, 2013



250 wapoteza maisha Pakistan 

ISLAMABAD, Pakistan
WATU zaidi ya 250 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi lililopiga Kusini Magharibi mwa nchini humo.
Wakielezea tetemeko hilo viongozi wa eneo hilo walisema limesababisha madhara makubwa kwa wananchi ambao wengi hawana makazi baada ya nyumba zao kubomoka.
Serikali ya Pakistan imeweka wazi kuwa inaendelea kuhakikisha inatoa msaada kwa waathirika pamoja na kuchukua hatua kuhakikisha wanarejesha hali ya mambo kama ilivyokuwapo hapo awali.
Serikali ya jimbo la Balochistan imetangaza hali ya hatari katika wilaya ya Awaran ambayo imeathiriwa zaidi na tetemeko hilo.
Kwa mujibu wa mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa ya nchi hiyo, tetemeko hilo linakadiriwa kuwa nguvu ya 7.7 ukubwa wa richa.
Jeshi limeendelea na harakati za uokoaji katika eneo hilo ambapo inahofiwa kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka zaidi kutokana na kuhofiwa kuwepo kwa wengine ambao watakuwa wamefukiwa katika majengo yaliyoporomoka.
Makundi ya wapiganaji waliojihami kwa silaha yameendelea kuwa changamoto katika wakati huu, ambako juzi watu wenye silaha waliripotiwa kuwashambuliwa wahudumu wa afya wanaowahudumia waathirika wa tetemeko hilo.
Tetemeko hilo la ardhi limechangia kuharibiwa kwa huduma za mawasiliano na wasiwasi umeendelea kutanda kwenye majiji mengine kama vile New Delhi na Dubai ambayo yanahofia huenda yakakumbwa na tetemeko kama hilo.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text