TB imetokana
na mwafrika
KIKUNDI cha
wanasayansi wa kimataifa kinasema kuwa homa ya mapafu(TB) ilitokana na waafrika
waliokuwa wana hama hama miaka 70,000 iliyopita.
Utafiti wa
wanasayansi hao imekwenda kinyume na dhana kwamba homa ya Mapafu ilitokana na
wanyama miaka 10,000 iliyopita na kusambaa hadi kwa binadamu.
Utafiti huo
unaonyesha uhusiano mkubwa ulioko kati ya historia ya binadamu na homa ya
mapafu au TB.
Ugonjwa huo
husababisha zaidi ya vifo milioni moja kila mwaka.
Utafiti wa
awali ulionyesha kuwa homa ya mapafu ambayo huwaathiri wanadamu ilianza
kusikika miaka 10,000 iliyopita wakati idadi ya watu ilipoanza kuongezeka huku
wengi wakianza kufanya kilimo.
Watafiti
walikusanya taarifa za kijiografia kuhusu vinasaba vya watu kutoka kwa aina 259
ya vimelea vya homa ya TB kwa lengo la kufananisha na historia ya binadamu
Afrika.
Profesa
Sebastian Gagneux, kutoka katika taasisi ya magonjwa ya kiafrika nchini Uswizi
alisema kuwa, walichogundua ni kuwa binadamu wa kwanza alitokea Afrika sawa na
maambukizi ya kwanza ya Kifua Kikuu kuripotiwa miaka 60,000 iliyopita,
ikisemekana kuwa mapema mno ikilinganishwa na ilivyodhaniwa.
''Lengo letu
ni kutaka kuthibitisha kuwa ugonjwa wa kifua kikuu ulianza kuenea miongoni mwa
binadamu na baadaye kuenea kwa wanyama,”' alisema Profesa Sebastaian.
Swali sasa
ambalo wanasayansi wanahoji ni vipi vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu viliweza
kudumu kwa miaka 60,000 miongoni mwa watu wachache sana.
Moja ya
mambo yanayowashangaza wanasayansi ni kuwa mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huo
kwa miaka mingi kabla ya kuanza kuonyesha dalili za kuambukizwa.
Hali ya
ugonjwa huo kukaa kwa miaka mingi bila ya kuonyesha dalili ndiyo inawafanya
watafiti kuamini kuwa sababu kuu ya ugonjwa kudumu kwa muda huo mrefu.
Wakati idadi
ya watu ilipoanza kuongezeka ugonjwa huo nao ukaanza kusambaa.
Na wakati
watu walipoendelea kuongezeka ndipo ugonjwa huo nao ulipoendelea kuenea.
Hatua
itakayofuata katika utafiti wa wanasayansi hawa ni kutumia data za vinasaba vimelea
vya TB vilivyo weza kudumaa kwa miaka mingi kabla ya kujitokeza kama ugonjwa
mwilini mwa mtu.
Ugonjwa wa
Kifua Kikuu ni tisho kubwa duniani kwa kusababisha vifo milioni 1.4 mnamo mwaka
2011, kulingana na shirika la afya duniani.
Ikiwa
wanasayansi wanaweza kuelewa uhusiano uliokuwepo kati ya ugonjwa wa TB kwa wanadamu,
inaweza kusaidia katika juhudi za kupunguza maambukizi yake.
0 comments:
Post a Comment