Seseme: nitafanya mauaji Bilcanas
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya Seseme Haji ‘Spince Seseme’ amewataka mashabiki wake
kuja kwa wingi kushuhudia shoo yake anayotarajia kuifanya katika ukumbi wa
kimataifa Afrika Mashariki, Club Bilcanas siku ya jumapili.
Seseme
anayetamba na kazi zake zinazokwenda kwa jina la ‘Ayaya’ na ‘Zinawauma’ amesema
amepania kupiga shoo ambayo haitasahaulika kwa wapenzi wa burudani watakao
hudhuria katika shoo hiyo.
Alisema
kuwa ili kuhakikisha shoo yake inakuwa nzuri na ya kuvutia atahakikisha jukwaani
anaingia kushambulia sambamba na wacheza shoo wake wake wanaocheza staili
mbalimbali tofauti za kuvutia na za kisasa.
Seseme
pia aliwaahidi mashabiki watakaofika hapo kuwaonjesha wimbo wake mpya
unaokwenda kwa jina la ‘Sinderela’ utakaokuwa ‘surprise’ kwa rafiki yake mkubwa
wanayeshirikiana naye katika kazi za muziki ambaye naye atamuweka hadharani kwa
wale watakaohudhuria.

0 comments:
Post a Comment