Uhuru Kenyatta ahakikisha serikali
imara
RAIS wa
nchini hapa, Uhuru Kenyatta amewahakikishia wakenya kuwa uongozi wa serikali
yake utaendelea kuwahudumia wakenya, licha ya kuwa na kesi zinazomkabili na makamu
wake William Ruto katika mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) jijini
Hague huko Uholanzi.
Kesi hiyo
ambayo pia inamshirikisha mwanahabari Joshua Arap Sang inahusiana na vurugu
zilizotkea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Rais
Kenyatta amewataka wakenya kutokuwa na hofu kutokana na maneno ya watu
wanaotaka kutumia nafasi hiyo kueneza uvumi kuwa Kenya haitakuwa na uongozi
ikiwa rais Kenyatta na makamu wake watakapo elekea huko Hague badala yake
amewaambia kuwa wao hawana hatia na anaamini watashinda na ushindi huo utakuwa
wa wakenya.
Wakati hayo
yakijiri jijini Nairobi huko Mombasa mdahalo kuhusu hatua ya wabunge wa Kenya
kupitisha hoja ya kutaka taifa hilo kujitoa katika mkataba wa Roma uliobuni
mahakama ya kimataifa ya ICC, bado unaendelea kupingwa na wananchi wakiwemo
viongozi mbali wa kisiasa nchini humo.
Makamu wa
zamani wa rais Kalonzo Musyoka amesema kuwa suala la kujiondoa katika mkataba
wa Roma unaitangaza vibaya nchi hiyo kimataifa.
Rais Kenyata
na makamu wake William Ruto wamepangiwa kuhudhuria baadhi ya vikao vya kesi zao
kwa pamoja baadaye mwezi huu ambapo Ruto anatarajia kuondoka nchini Kenya leo
kuelekea Hague Uholanzi ambapo rais Kenyatta atafuata baadaye.
0 comments:
Post a Comment