Wafuasi wa
Morsi wafungwa jela
WAKATI
aliyekuwa rais wa nchini hapa, Mohammed Morsi akiwa katika kizuizi
kisichojulikana akisubiri kufunguliwa mashtaka wafuasi wake watano wamefungwa
kifungo cha muda mrefu jela.
Hukumu
hiyo imetolewa na mahakama ya kijeshi ya Misri baada ya kuwapata na hatia ya
kushambulia wanajeshi.
Mmoja
wa wafungwa hao alifungwa jela maisha, wengine watatu wakipewa vifungo vya kati
ya miaka 5, 15 na 45, kwa mujibu wa taarifa za jeshi.
Walishtakiwa
kwa kosa la kuwafyatulia risasi wanajeshi wakati wa ghasia na vurugu katika mji
wa bandarini ya Suez mwezi uliopita.
Vurugu
hizo zilitokea baada ya msako mkali uliofanywa na maofisa wa usalama dhidi ya
wafuasi wa Moris waliokuwa wamepiga kambi mjini Cairo.
Mamia
ya wanachama waliofanya vurugu za Muslim Brotherhood, waliuawa wakati wafuasi
wa Morsi walipokuwa wamepiga kambi nje ya msikiti wa Rabaa al-Adawiya na katika
uwanja wa Nahda wakitaka Morsi aachiwe, ingawa waliondolewa kwenye kambi hizo
Agosti 14.
Vurugu
zilizotokea mjini Suez, Mashariki mwa Cairo, kati ya Agosti 14 na 16 zilisababisha
vifo vya zaidi ya watu 30.
Hata
hivyo haijulikani ikiwa wale waliohukumiwa Jumanne ni wanachama wa Brotherhood.
Lakini
ikiwa ni wanachama wa Muslim Brotherhood, hukumu walizopewa bila shaka
zitaathiri chama hicho hasa ikizingatiwa ni za kwanza kutolewa na chama hicho tangu
kuondolewa mamlakani kwa Morsi.
Viongozi
wa mashtaka walitangaza Septemba mosi, miezi miwili baada ya kuzuiliwa kwa
Morsi kuwa anatufunguliwa mashtaka kwa kuchochea mauaji.
0 comments:
Post a Comment