Wanamgambo
50 Boko Haram wauwawa
JESHI nchini
hapa limesema kuwa limewaua wanamgambo 50 wa kundi la Boko Haram kwenye
operesheni iliyozinduliwa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo katika kukabiliana
na mashambulizi ya waasi, kwenye vurugu za karibuni kulikumba eneo hilo.
![]() |
| kikosi cha Boko haram |
Taarifa
kutoka kwa wakazi zinasema wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wanatoka katika
madhehebu ya kiislam yenye vurugu walifyatua risasi kwenye soko siku ya
Alhamisi katika mji wa Gajiran, na kuua watu 15.
Msemaji wa
jeshi Sagir Musa amewaambia waandishi wa habari mjini Maiduguri kwamba jeshi
lilituma vikosi vya askari katika kukabiliana na azma ya washambuliaji ambapo
kwa msaada wa vikosi vya anga waliweza kushambulia kambi za wanamgambo hao na
kufanikiwa kuwaua 50
Mgogoro wa
Boko Haram unakadiriwa kugharimu maisha ya zaidi ya watu 3,600 tangu mwaka
2009, ikiwa ni pamoja na mauaji yaliyotekelezwa na askari wa vikosi vya
usalama, ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

0 comments:
Post a Comment