Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, October 13, 2013

AU: Kenyatta, Bashir wasihudhurie kesi ICC

ADDIS ABABA, Ethiopia
VIONGOZI katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU),  wametaka kesi inayoendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta icheleweshwe kwa ajili ya kutoa muda kwa kiongozi huyo kuendelea na majukumu ya kuwahudumia wananchi wake.
Maamuzi hayo yamefikiwa jana kwenye mkutano uliofanyika jijini hapa na kuwashirikisha viongozi wa Afrika ambao wameishutumu mahakama ya ICC kuwa wamekuwa wakilenga zaidi viongozi wa bara la Afrika katika kesi zake.
AU imeunga mkono azimio linaloitaka ICC kutomshtaki kiongozi yeyote wa barani Afrika na kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya Kimataifa wakati akiwa madarakani.
Mkutano huo ulizungumzia pia suala la Afrika kufikiria kujiondoa kutoka ICC ambapo jambo hilo halikuungwa mkono na wanachama wa kutosha.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia ambaye ni mwenyekiti wa baraza kuu la AU, Tedros Adhamom Ghebreyesus, amesema kuwa Umoja wa Afrika hauna mamlaka ya kumzuia kiongozi wa taifa lolote kushtakiwa mjini The Hague ila jambo wanalofanya ni kuwasiliana na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kulitaka kutoa idhini kwa kesi ya Kenyatta kucheleweshwa kabla ya mashitaka yake kuanza rasmi Novemba 12.
Ghebreyesus akizungumzia iwapo kama uamuzi huo hautachukuliwa basi viongozi wa Afrika watachukua uamuzi wa kumzuia Kenyatta kuhudhuria katika mahakama hiyo mjini The Hague.
Alisema kuwa uamuzi huo wa kutoshtakiwa kwa viongozi walioko madarakani hautaishia kwa Kenyatta pekee bali hata kwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir ambaye pia anatakiwa kufika hapo kwa makosa ya uhalifu wa kivita.
Maamuzi hayo yamepingwa na makundi ya kutetea haki za binaadamu, kutoka nchini Kenya ambako, Naibu mkurugenzi mkuu wa Tume ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Kenya (KHRC), Davis Malombe alipinga wito huo wa AU wa kutaka kesi hiyo kucheleweshwe akisema “ni jaribio jingine la kuvuruga na kuchelewesha haki kwa waathiriwa wa Kenya na unasaliti madai ya ahadi ya AU ya kupambana na ukwepaji sheria”.
Baada ya kuwasili mjini Addis Ababa, kabla ya kikao, Rais Kenyatta alitoa hotuba iliyokuwa na maneno makali, akiishutumu ICC kuwa ni wakala wa himaya ya kibeberu inayosambaratika.
Alisema “Hata ingawa tuliongozwa na kudhibitiwa na mabeberu kwa maslahi ya kikoloni katika miaka iliyopita, sasa hivi Afrika ni mataifa ya kijivunia na yaliyo na uhuru. Zaidi ya yote, hatima yetu iko mikononi mwetu. Hivyo ni muhimu kwetu kuwa macho dhidi ya mifumo inayoendelea kuwekwa na watu wa nje, wenye nia ya kuidhibiti hatima yetu”.
Rais huyo wa Kenya aliupongeza Umoja wa Afrika kwa kumuunga mkono huku akisema “Nikiwa kama Rais wa Kenya, inanifanya nijivune kwa kuutegemea Umoja wa Afrika kwa kunisikiliza na kunisaidia wakati wa matatizo hivyo naamini Afrika imesimama na mimi”.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) si chombo cha kutekeleza uadilifu bali ni mahakama ya kibaguzi na mwanasesere wa madola ya kibeberu.

REUTERS

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text