Wahamiaji
haramu 50 wafariki bahari ya Mediterranean
MALTA,
Italia
BOTI
iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu wanaokadiriwa kufikia 200 imezama katika
bahari ya Mediterranean na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50 katika kisiwa
cha Malta vya nchini hapa.
Tukio
hilo la boti kuzama limetokea umbali wa takribani kilometa 120 kutoka Lampedusa
na takribani kilometa 110 kutoka visiwa vya Malta.
Serikali
ya Malta na Italia wanashirikiana kufanikisha kazi ya uokoaji kwa kutumia helikopta
na meli kwa ajili ya kuwabeba manusura wa ajali hiyo ili kuwafikisha katika
eneo la nchi kavu.
Kwa
mujibu wa takwimu za Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR),
Italia ina wahamiaji haramu wanaofikia 32,000 ambao wamewasili Kusini mwa
Italia na Malta kwa mwaka huu na tayari theluthi mbili wameomba kupewa uraia wa
nchi hiyo.
Wahamiaji
wengi zaidi waliowasili mwaka huu wamekuwa wakikimbia machafuko yanayoendelea
nchini Syria na wengine wametokea katika mataifa ya Kaskazini mwa Africa.
Takwimu
zaidi zinasema kuwa kuna zaidi ya wahamiaji 20,000 wamekufa maji katika kipindi
cha miaka 20 iliyopita wakiwa katika harakati za kuingia barani Ulaya kwa lengo
la kutafuta hifadhi na maisha bora.
Tukio
hilo limetokea ikiwa ni wiki moja kupita baada ya boti nyingine iliyokuwa na
wahamiaji haramu kutoka barani Afrika kuzama na kusababisha vifo vya watu zaidi
ya 300 karibu na visiwa vya Lampedusa Kusini mwa Italia.

0 comments:
Post a Comment