Kenyatta: Nitahudhuria kesi ICC
NAIROBI, Kenya
RAIS wa nchini
hapa, Uhuru Kenyatta amesema kwamba yuko tayari kuhudhuria kesi ya jinai inayomkabili
katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), Hague Uholanzi baada ya mahakama hiyo kumruhusu kutohudhuria
kwa baadhi ya vikao.
Akizungumzia
hilo juzi, Rais Kenyatta aliishukuru ICC kwa kukubalina na uamuzi huo aliouona
kama kujali maslahi ya Wakenya kwa kutoa muda kwa rais wao kuwaongoza badala ya
kukaa kila kikao cha kesi yake huko Hague, hali itakayosababisha kukosekana
muda wa kuwaongoza Wakenya.
Rais Kenyatta
ameahidi kushirikiano na mahakama hiyo hadi mwisho wa kesi yake, kwa kuhudhuria
baadhi ya vikao atakapokuwa akipata muda na kikao cha kwanza atakachohudhuria
kitakuwa ni cha ufunguzi Novemba 12 na baadaye atarudi nchini Kenya.
Ingawa bado
kuna taarifa zinaeleza kuwa itakuwa vigumu kwa Rais huyo kwenda Hague kutokana
na viongozi wengi wa Kenya kuliona jambo hilo kama kumsababishia kiongozi wao
kuonekana lege lege.
The Kenyan Daily
Post
0 comments:
Post a Comment