Majeshi ya Ujerumani yaondoka Kunduz
BERLIN, Ujerumani
VIKOSI vya
jeshi la Ujerumani (Bundeswehr), vimeondolewa kutoka jimbo la Afghanistan la
Kunduz baada ya kukaa kwa muda wa miaka 10 vikifanya operesheni ya kulinda
usalama wa nchi hiyo.
Akizungumzia
hatua hiyo juzi, Luteni kanali Heiko Diehl alisema kuwa wamefikiwa hatua hiyo
ikiwa ni nia yao ya kuondoa majeshi ya NATO nchini humo baada ya kukamilika kwa
opereshani yao.
Alisema kuwa
“Tumekamilisha kwa mafanikio makubwa operesheni hii hivyo tumeona tujiondoe
hasa baada ya kuwasili katika Mazar-i-Sharif na kuona hali ni shwari.
Kuondoka kwa
vikosi hivyo vya Ujerumani kumepongezwa na kamanda wa eneo hilo wa jeshi la
kimataifa linaloongozwa na NATO linalotoa msaada wa usalama kaskazini mwa
Afghanistan, Meja jenerali Jörg Vollmer aliyejivunia mafanikio waliyofikia.
Alisema "Tunajivunia
kile wanajeshi wetu walichofanikisha katika jimbo la Kunduz tangu walipo anza
hadi walipofikia,"
Kabla ya
kuondoka rasmi juzi jeshi la Ujerumani Bundeswehr lilikuwa limeshakabidhi kambi
yao kwa jeshi la usalama la Afghanistan katika sherehe iliyofanyika Oktoba 6.
REUTERS
0 comments:
Post a Comment