Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, October 20, 2013

Upinzani Guinea wajiandaa kwenda mahakamani
 

GUINEA-BISSAU, Guinea  
WAPINZANI nchini hapa wanatarajia kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge yaliyotangazwa hivi karibuni ambayo yaliyokipa ushindi chama tawala cha RPG kinachoongozwa na Rais wa nchi hiyo Alpha Conde.
Msemaji wa muungano wa wapinzani Sydia Toure amesema kuwa kamwe hawawezi kutambua matokeo ambayo hayawakilishi matakwa ya wananchi wa Taifa hilo.
Kauli iliyoungwa mkono na mpinzani mkuu wa Rais Conde toka chama cha UDFG Cellou Dalein Diallo aliyesema kuwa wana uthibitisho wa kutosha juu ya udanganyifu uliofanyika katika uchaguzi huo.
Hatua hiyo ya wapinzani imezusha hofu kuwa huenda machafuko yakalikumba Taifa hilo lenye historia ya migogoro ya kisiasa na kijeshi na umwagaji damu kwa waandamanaji.
Mkuu wa Umoja wa Taifa katika mataifa ya Magharibi mwa Afrika, Said Djinnit ametoa wito kwa wapinzani kutafuta haki yao kwa kuzingatia misingi ya sheria na kuwa watulivu wakati wakisubiri maamuzi ya mahakama juu ya uhalali wa matokeo hayo.
Msemaji wa serikali Damantang Albert Camara amesema chama tawala kimeridhishwa na matokeo hayo ambayo yamehitimisha mchakato huo uliochukua muda mrefu kumalizika.
Hata hivyo waangalizi wa uchaguzi huo toka taasisi mbalimbali za kimataifa Oktoba 9, walisema kulikuwa na dosari ngingi zinazoathiri uhalali wa matokeo ya uchaguzi huo.
Katika matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi siku ya ijumaa, chama tawala cha RPG pamoja na vyama vingine shirika walipata jumla ya viti 70 kati ya 114 vya bunge zima, ambapo RPG pekee ilipata viti 53 na washirika wake walipata 7.
Chama pinzani cha UFDG kinachoongozwa na Cellou Dalein Diallo kilipata viti 37 wakati chama cha Waziri Mkuu wa zamani nchini humo Sidya Toure cha UFR kilipata viti 10 na nafasi nyingine zilizobaki  zilikwenda kwa vyama vidogo vilivyoshiriki uchaguzi huo.

Matokeo hayo yametangazwa ikiwa ni wiki tatu baada ya tukio la upigaji kura kufanyika, suala ambalo lilizidisha hofu kuwa huenda udanganyifu unafanyika ili kukipa ushindi chama tawala.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text