Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Wednesday, October 9, 2013

Rais Obama awaangukia wabunge Republican kupitisha Bajeti

WASHINGTON, Marekani
RAIS wa nchini hapa Barrack Obama amesema kuwa yuko tayari kuzungumza na wabunge wa Republican kuhusu kupitishwa kwa bajeti muhimu ili kurejesha huduma za serikali zilizokwama tangu wiki iliyopita.
Uamuzi wa Rais Obama unaonekana kutaka kuondoa doa lililopangwa kuwekwa kwenye uongozi wake katika nyanja ya kiuchumi.
Kauli hiyo imetoka baada ya wiki iliyopita, kuripotiwa kuwa maelfu ya wafanyakazi wa Serikali nchini humo walirudi majumbani baada ya kukosa kazi kwa kutokuwepo kwa fedha za kufanikisha huduma muhimu za serikali baada ya wabunge wa Republican kukataa kupitisha bajeti hiyo muhimu.
Wabunge wa Republican wakiongozwa na Spika wa Congress John Boehner wamesema kuwa wao wako tayari kwa mazungumzo lakini walisikitishwa na hatua ya rais Obama kukataa kuzungumza nao.
Rais obama 
Boehner ameongeza kuwa hatua ya rais Obama kuwataka wao kujisalimisha na kukubali sera zake ni hatari kwa uchumi wa Marekani ambao huenda ukadorora ikiwa suluhu halitapatikana kufikia Oktoba 17, mwaka huu kwa sababu serikali itafikia mwisho wa kukopa fedha.
Rais Obama kwa upande wake amemjibu Spika Boehner kwa kumwambia kuwa ana uwezo wa kufungua huduma za serikali kwa kuruhusu wabunge wa Congress kupiga kura kuamua ikiwa wanataka huduma za serikali zirejelewe au la.

Wabunge wa Republican wanasema kuwa walichukua hatua hiyo, ili kuchelewesha sera ya raia Obama kuhusu bima ya afya, mpango ambao rais Obama ameendelea kusisitiza kuwa hautabadilishwa.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text