Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, October 13, 2013


Mwandishi ITV apigwa risasi

MTU mmoja anayedaiwa kuwa mchumba wa Ufoo Saro aliyefahamika kwa jina la Ateri Mushi, amempiga risasi na kumjeruhi mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro na kumuua mama mzazi wa mwandishi huyo, Anastazia Saro na kisha kujipiga risasi mwenyewe.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Ruben Mchome alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Alisema kuwa mwanaume aliyefanya mauaji hayo alikuwa anafanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini Sudan kama ofisa katika kikosi cha Sudan.
Kamanda Wambura amesema inasemekana kulikuwa kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro.
Alipofika huko inadaiwa kuwa mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba anamtetea mwanaye yaani Ufoo Saro, ndipo mwanaume huyo alipotoa bastola na kumpiga mama wa Ufoo Saro risasi kifuani na kumuua papo hapo na kisha akampiga Ufoo Saro risasi ya mbili, moja ya tumboni na nyingine mguuni.
Inaelezwa kuwa baada ya kudhani kwamba amewaua wote, ndipo naye alipojifyatulia risasi kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
Nukuu nyingine kutoka kwenye mitandao jamii zinasema, akizungumza kwa njia ya simu, Steven Chuwa wa ITV amesema tukio hilo limetokea kwenye nyumba alikokuwa akiishi mama wa Ufoo Saro, Kimbamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa  Ufoo alikimbizwa katika hospitali teule ya Tumbi (Kibaha) katika jitihada za kuuokoa uhai wake na baadaye alihamishiwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kitengo cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).
Taarifa nyingine zinasema Mushi aliwasili nchini jana na  kufikia nyumbani kwa Ufoo alfajiri ya leo na kisha wawili hao ndipo walipoondoka kuelekea nyumbani kwa mama mzazi wa Ufoo ili kutafuta suluhu.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text