Republican kumpinga Obama kuhusu Iran
WASHINGTONG,
Marekani
MASENETA
kadhaa wa chama cha Republican katika Congress ya Marekani wamesema
watawasilisha muswada wa kuiwekea vikwazo zaidi Iran kufuatia ripoti kuwa
serikali ya Rais Barack Obama inafikiria pendekezo la kuirejeshea Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran mali zake zenye thamani ya mabilioni ya dola zilizokuwa
zimezuiliwa na Washington.
Hayo
yameelezwa na gazeti la New York Times liliripoti kuwa serikali ya Marekani
inapanga kuzirejesha mali za Iran kama hatua ya kuifanya Tehran nayo ichukue
hatua ya kuwa na imani na serikali ya Washington katika uhusiano wao
wanaotaraji kuuanzisha kuhusu miradi ya Iran ya nyuklia.
Hata hivyo
Maseneta Lindsey Graham, Kelly Ayotte na Mark Kirk kutoka chama cha Republican
wametoa taarifa wakitaka serikali ya Obama iiwekee vikwazo zaidi Iran.
Baada ya
mazungumzo ya Geneva, serikali ya Marekani ilisema kuwa mazungumzo hayo ya nyuklia
kati ya Iran na kundi la 5+1 yaliyofanyika Oktoba 15 na 16 yalitoa mwanga wa
matumaini.
Inafaa kukumbusha hapa kuwa Marekani na Umoja wa
Ulaya zimeiwekea vikwazo vya uchumi vya upande mmoja Iran kwa kutumia
kisingizio cha tuhuma zisizo na ushahidi kwamba Tehran ina nia ya kuunda silaha
za nyuklia madai ambayo yamekanushwa mara kadhaa na Jamhuri ya Kiislamu
0 comments:
Post a Comment