Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, November 3, 2013



Jeshi Kenya laua Al Shabab 30

NAIROBI, Kenya
al Shabab kazini
WANAMGAMBO 30 wa kundi la kigaidi la Al Shabab wameuawa nchini Somaia katika oparesheni ya pamoja ya Jeshi la Kenya iliyoshirikisha askari wa serikali ya Somalia nje ya mji wa Kolbiyo ulio katika mkoa wa Lower Jubba ulio karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.
Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF)  Emmanuel Chirchir, oparesheni hiyo ya juzi ilichukua muda wa saa nzimana kuua wanamgambo 30 wa Al Shabab.
Hatahivyo msemaji wa Al Shabab amekanusha ripoti ya kuuawa wapiganaji wa kundi hilo na badala  yake amedai kuwa wamewaua wanajeshi  wanne wa upande wa pili katika mapigano hayo.
Mji wa Kolbiyo umekuwa ukitumiwa na wanamgambo wa Al Shabab kutekeleza mashambulizi ndani ya ardhi ya nchi ya Kenya kwa muda wakiitaka Kenya kuondoa vikosi vyao nchini humo.
Alhamisi Jeshi la Ulinzi la Kenya lilitangaza kuwa lilitekeleza shambulizi la angani ndani ya Somalia na kuharibu kambi ya mafunzo ya wanamgambo wa al Shabab waliohusika na hujuma dhidi ya jengo la maduka la Westgate mjini Nairobi Septemba mwaka huu.
KDF imemtoa taarifa iliyosema kuwa kambi hiyo ilikuwa na wapiganaji 300 ambao baadhi waliwaua na wengine kujeruhiwa.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text