Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, November 3, 2013



Vyama vya Tunisia vyashindwa kumteua waziri mkuu

TUNIS, Tunisia
CHAMA tawala nchini hapa, Ennahda pamoja na vyama vingine vya upinzani vimeshindwa kufikia muafaka kuhusu nanai anastahili kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.
Kushindwa huko kukubaliana kumechangiwa na pande zote mbili zilizokuwa zimekaa kikao cha faragha mwishoni mwa wiki mjini Tunis lakini hakuna mapatano yaliyofikiwa.
Kuna mvutano kuhusu vigogo wawili, Mohammad Ennaceur (79), anayeungwa mkono na upinzani na Ahmad Mestiri mwenye umri wa miaka 88 ambaye anaungwa mkono na Ennahda.
Atakaye chaguliwa kuwa waziri mkuu atakuwa na jukumu la kuunda serikali ya muda ambayo inapaswa kuwa na watu wasiopendelea upande wowote ili kuitayarisha nchi hiyo kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Tunisia ilitumbukia katika machafuko mwaka 2011 baada ya kuondolewa kwa utawala wa dikteta wa zamani Zine El Abidine Ben Ali kufuatia mwamko wa wananchi.
Mgogoro wa kisiasa ulipamba moto Tunisia baada ya kuuawa mwanasiasa mwandamizi wa upinzani nchini humo Julai mwaka huu.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text