Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, November 10, 2013




Ray C: Juhudi za Rais JK ziungwe mkono
Na Shehe Semtawa
MSANII wa muziki wa kizazi  kipya Rehema Chalamila ‘Ray C’ amwewataka viongozi mbalimbali nchini kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete za kupambana na kutokomeza janga la uingizaji na utumiaji wa mihadarati kwa vijana.
Ray C, aliyabainisha hayo jijini Dar es Salaam juzi, alipokuwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sigini, alipotembelea Kituo cha Tiba cha Dawa za Kulevya (Methadone Wing).
Alisema anaamini kuwa endapo viongozi waliokabidhiwa dhamana wataziunga mkono kwa dhati juhudi hizo zilizoanzishwa na rais za kupambana na janga hilo, anaamini mafanikio ya kulitokomeza yanaweza kupatikana haraka.
“Leo tarehe nane natimiza mwaka tangu nianze kutumia methadone hivyo nimeamua kufanya sherehe ndogo na wenzangu  ‘Rafiki’ katika kituo hiki, nimenunua vinywaji baridi na vitafunwa kidogo kwa ajili ya kufurahi pamoja”alisema Ray C.
Aidha, Ray C, aliitaka serikali kuongeza jitihada za mapambano yake kwani janga hilo ni kubwa nchini kutokana na ukweli kwamba wapo hata baadhi ya vigogo wanaotumia uraibu huo.
“Sasa najisikia vizuri na mshukuru baba (Rais), kwa kunishauri pamoja na jitihada zake za kuwaleta Wamerekani katika kutupatia tiba hii ambayo imenirudisha katika hali yangu ya kawaida hadi nikaweza kuingia tena studio kurekodi nyimbo tena ni jambo kubwa sana”alisema Ray C.
Alitoa rai kwa wasanii wenzake, na baadhi ya watu maarufu ambao anaamini wapo na tayari wamekwisha athirika na utumiaji wa mihadarati kuwa wasione aibu wajitokeze katika kituo hicho kwani dawa ya methadone inaponesha, “Wafike tu watapona kama mimi”alisisitiza Ray C.
Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Sagini, aliiagiza Manispaa ya Kinondoni kuangalia uwezekano wa kuwapatia ajira baadhi ya vijana hao kutokana na elimu waliyonayo kwani katika kundi hilo walikuwepo hata wasomi wa elimu ya chuo.
Dk. Elias Mrita, alisema hadi sasa kunawagonjwa 375 ambao hupatiwa matibabu, na wapo ambao tayari wamekwishapona, aliongeza kuwa kituo hicho kinaendeshwa kwa msaada wa serikali ya Marekani.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text