Sitaki kuiona chadema ikifa kizembe
![]() |
| Dk. Slaa nyuma akiteta jambo na Freeman Mbowe, Zitto Kabwe |
UNAPOZUNGUMZIA
chama ambacho kwa sasa ni gumzo na kinaipeleka puta Chama Cha Mapinduzi (CCM), na
kuwafanya viongozi wake washindwe kunywa maji na kukosa usingizi si kingine
bali ni chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Lakini
katika siku za hivi karibuni nimeanza kupata shaka kuhusu muenendo wa chama hicho
kutokana na hali ya kutoelewana ambayo imeanza kujitokeza kwa baadhi ya vijana
wake ambao wamekuwa na mvuto mkubwa kwa Wapenzi na mashabiki wa chama hicho.
Ingawa wengi
wamekuwa hawazipatii uzito unaostahili chokochoko hizo kwa kuhakikisha
wanazitafutia ufumbuzi mpaka inafikia mahali misuguano hiyo inatoka ndani ya
chama na hatimaye kuwafikia wananchi kwa kupitia vyombo vya habari na mitandao
ya kijamii hii ni hatari.
Sitaki
kuamini kwamba ni vibaya watu kufikia kuwa na migongano ya mawazo, lakini pindi
inapofikia mahali migongano hiyo inatoka nje ya vikao halali vya chama huwa ni
hatari kwa mustakabari wa chama husika na mageuzi kwa ujumla.
Naamini bado
Watanzania tulio wengi hatujasahau kilicho tokea kwenye chama cha NCCR- Mageuzi
chama kilichoaminika kuwa mzizi Mkuu wa mageuzi nchini miaka ya 1990.
Chama hiki
kilitokana na kamati iliyoundwa Juni 12, 1991, wakati huo ikijulikana kama
National Committee for Constitutional Reform ama kwa kifupi NCCR, ambayo
Februari 15, 1992 iligeuzwa kuwa chama cha siasa, kilichoitwa National
Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR-Mageuzi).
Chama hicho
kilipata nguvu ya ajabu katika uchaguzi wa mwaka 1995, Lakini siku zilivyopita,
chama hicho kilikumbwa na mgogoro kwa viongozi wake kutofautina kimtazamo, ambapo
Marando aliingia katika mgogoro na Mwenyekiti wake wa wakati huo, Augustine
Mrema.
Hali hiyo
ilifanya chama kikagawanyike kwa kundi moja lililokuwa na wajumbe wengi wa
Kamati Kuu likimuunga mkono Marando huku Mrema akiwa na wanachama wengine
waliokuwa nyuma yake.
NCCR-Mageuzi
ikagawanyika kwa makundi mawili ambako kundi la Marando lilihama kutoka ofisi
za Makao Makuu zilizokuwa eneo la Argentina, Manzese na zikafunguliwa mpya
maeneo ya Posta mpya jijini Dar es Salaam.
Mgogoro huo
uliendelea hadi katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika katika hoteli ya
Raskazone mkoani Tanga, ambapo vituko vilitawala, vikiwemo vipigo na vitisho
vya kuuana na hata Mrema alipoona NCCR-Mageuzi yamemshinda, aliondoka katika
chama hicho na kujiunga na Chama cha Tanzania Labour (TLP).
Hayo ni
baadhi ya mambo ambayo nilitaka kukumbusha kidogo, ili iwe fundisho kwa Chadema
ambao wamekuwa wakiona kila linalotokea na kulidharau hivyo sitaki kuona
yanawakuta yaliyokipata Chadema.
Mgogoro
unaoendelea hivi sasa ukiwahusisha Zitto Kabwe na Godbless Lema usichukuliwe
kijujuu na kudharauliwa yasije yakawakuta yaliyokikuta NCCR-Mageuzi.
Hali iliyonifanya
nione mgogoro huo unaweza ukatoa taswira mbaya ni taarifa ambayo Zitto ameitoa
hivi karibuni akijaribu kujibu taarifa inayoelezwa kutolewa na chadema ikiwa na
kichwa cha habari "Taarifa ya Siri ya Chadema"
Sehemu ya
taarifa hiyo anasema nilipokuwa katika ziara ya bara la Ulaya kati ya Oktoba 21
mpaka Novemba 2 mwaka huu, nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa
"Taarifa ya Siri ya Chadema" ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika
mitandao mbalimbali ya kijamii.
“Taarifa ya
Chadema inasema kwamba chama hicho (chama changu) kilikuwa kimechunguza
mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha
kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema.
Ripoti hiyo
ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes ambaye, kwa
mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000
za Marekani kupitia kwenye akaunti yake binafsi. Taarifa hii ya kutunga na
iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha, imenifadhaisha, kunisikitisha na
kunikasirisha.
Taarifa hii
iliibuliwa katika kipindi ambacho nilikuwa safarini kutetea haki za Watanzania
na Waafrika ambao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache
waliohifadhi mali katika nje za nje na pia kupigania makampuni ya mataifa
tajiri yalipe kodi stahiki katika nchi zetu.
Pengine
lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni kutaka kunipoteza kutoka katika nia na dhamira
yangu ya dhati ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao. Muda ambao
watunzi wa ripoti hiyo waliamua kutoa taarifa yao unazua maswali mengi kuliko
majibu.
Nafahamu
kwamba mimi ni mwanasiasa ambaye nimekuwa mlengwa (target) wa mashambulizi
kutoka kwa makundi mbalimbali ya wanasiasa na vikundi vyao. Kama mwanasiasa,
niko tayari kupokea changamoto zozote zinazokuja na uanasiasa wangu.
Hata hivyo,
ambacho sitakubali ni kwa watu kutumia jina langu na uanasiasa wangu kunichafua
mimi binafsi na watu wengine wasiohusika kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo
yao ya kidhalimu.
Raia huyo wa
Kijerumani tayari amekana kuhifadhi fedha zangu. Kwa maelezo yake kwa baadhi ya
viongozi wa Chadema amekana kuwa na akaunti inayotajwa na amekana pia kuwepo
nchini Ujerumani katika siku na wakati uliotajwa kwenye ripoti hiyo.
Ripoti hiyo
imemtaja pia Dk. Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ikidai
kwamba nilikutana naye na alishiriki kwenye igizo hilo la kunipa fedha.
Niseme
mapema kwamba tangu kuzaliwa kwangu sijawahi hata mara moja kukutana na Dk.
Kimei popote pale ndani au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye amejenga jina
lake kwenye taaluma ya kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la kumchafua Zitto
Zuberi Kabwe si uungwana bali ni unyama.
Kutokana na
uchafuzi huu wa wazi dhidi ya taswira yangu binafsi na watu wengine
walioingizwa kwenye mkumbo huu, nimeandika rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chadema,
Dk.Wilbrod Slaa kumwomba athibitishe kwamba kinachoitwa Taarifa ya Siri ya
Chadema ni kweli ni taarifa ya chama au kiikanushe ili niweze kuchukua hatua za
kisheria dhidi ya waandishi wa hekaya hiyo.
Cha ajabu,
nimepokea ujumbe wa kutishiwa maisha kutoka kwa mtu anayejiita Theo Mutahaba na
kuahidiwa kupotezwa endapo nitaendelea na jitihada zangu za kupambana na ufisadi
na kutafuta haki kwa Watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi,
kikanda, kikabila na kidini.

0 comments:
Post a Comment