Marekani:
Hatukwamishi amani ya Pakistan
WASHNGTON, Marekani
MAREKANI
imetupa madai ya kuihusisha na kutajwa kama kikwazo dhidi ya jitihada za mazungumzo
ya amani baina ya serikali ya Pakistan na wanamgambo wa Taliban.
Washington
imekanusha madai hayo ambayo yamechochewa na kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa
Tehreek-e-Taliban nchini Pakistan, Hakimullah Mehsud aliyeuawa katika shambulio
la ndege zisizokuwa na rubani mjini Waziristan wiki iliyopita.
Ikulu ya
Washington imeendelea kusisitiza kuwa wao wana lengo moja na Pakistan ambalo ni
kukomesha ugaidi.
Awali Waziri
wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Chaundry Nisar alilaumu mashambulizi hayo
yanayofanywa na vikosi vya Marekani na alilitaja shambulizi lililosababisha
kifo cha kiongozi huyo kama kizingiti kilichokuja siku chache kabla ya pande
hizo mbili kuanza mazungumzo.
Majeshi ya
usalama nchini Pakistan yapo katika tahadhari ya hali ya juu yakihofia huenda
Taliban ikalipiza kisasi baada ya kuuawa kwa kiongozi wao.
Katika hatua
nyingine Marekani imethibitisha kuwa Balozi wake Richard Olson amehojiwa na
Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan, ingawa haijaweka wazi kilichojadiliwa
katika mazungumzo hayo.
0 comments:
Post a Comment