Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Thursday, November 14, 2013




M23 wagawanyika mkataba wa amani DRC

KINSHASA, DRC
M23
KUNDI la waasi wa M23 la nchini hapa limeelezwa kugawanyika kuhusu kushindikana kwa utiliwaji wa saini mkataba wa amani kati yake na Serikali ya Kinshasa.
Hatua hiyo imefikia siku chache baada ya kuvuinjika kwa mazungumzo yaliyofanyika jijini Kampala yavunjike kwa kushindwa kutiliana saini hati ya makubalino waliyofikia kati ya wajumbe wa serikali ya DRC na kundi la M23.
Taarifa kutoka mjini Kampala zinasema kuwa kuna kundi jingine ambalo limejitenga kutoka kundi la waasi wa M23 ambalo lenyewe linaunga mkono mapendekezo yaliyokuwa yametangazwa na Serikali.
Taarifa iliyotolewa na kundi lililojitenga na M23, inasema kuwa wao hawaungi mkono madai ya wenzao na badala yake wanataka kukubaliana na Serikali ya DRC kuhusu kutiliana saini azimio la amani kwa mustakabali wa Wananchi wa Kongo.
Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Serge Kambasu Ngeve anayedai ni katibu mkuu wa kundi lililojitenga, inasema kuwa wao wako tayari kuzungumza na Serikali ya Kinshasa katika kutafuta njia muafaka za wao kusalimisha silaha na kutia saini azimio la amani.
Wakati hayo yakijiri Umoja wa Mataifa (UN) umeitaka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuandaa mpango kabambe wa kuhakikisha makundi mengine ya waasi wanasalimisha silaha ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha kwenye jeshi la nchi hiyo.
Tamko la UN linatolewa wakati huu ambapo kikosi maalumu cha umoja huo kilichoko mashariki mwa nchi hiyo ya DRC kwa kushirikiana na wanajeshi wa Serikali (FARDC) walifanikiwa kuwaondoa wapiganaji wa kundi la M23.
Operesheni hiyo ilifanikisha kumaliza uasi wa kundi la M23 uliokuwa umedumu kwa zaidi ya miezi 18 ambapo mamia ya watu wamepoteza maisha na wengine kuyakimbia makazi yao.
Naibu katibu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Kongo, Abdallah Wafi amewaambia wanahabari kuwa mpango huo ni muhimu kwa Serikali ya Kinshasa kama njia mojawapo ya kufikia suluhu ya amani mashariki mwa nchi hiyo.
Baadhi ya wapiganaji wa kundi la M23 walijisalimisha kwa vikosi vya Umoja huo na wengine kukimbilia Rwanda kuomba hifadhi jambo ambalo pia huenda likasababisha wapiganaji waliosalia na ambao hawajasalimisha silaha kujikusanya.
Katika hatua nyingine jeshi la Serikali ya DR Congo limesema hivi sasa linajipanga kuanza mashambulizi mapya dhidi ya wapiganaji wa Kinyarwanda wa kundi la FDLR ambao wakati fulani walipigana na Serikali mashariki mwa nchi hiyo.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text