Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Thursday, November 14, 2013



Marekani: Boko Haram, Ansaru ni magaidi

LAGOS, Nigeria
SERIKALI ya Marekani imeyataja makundi ya wapiganji wa kiislam ya nchini hapa ya Boko Haram na lile la Ansaru katika orodha yake ya ugaidi.
Kutokana na sheria za Marekani sasa itakuwa kosa la jinai kutoa msaada wowote kwa makundi hayo yanayotuhumiwa kusababisha vifo vya watu wengi nchini Nigeria.
Marekani imesisitiza kuwa hii ni hatua muhimu katika kuisaidia Nigeria na mashambulizi kutoka katika makundi hayo mawali na kwamba sasa yatambulike kama makundi ya kigaid kama ilivyo kwa lile la Al Qaeda.
Kutokana na hatua hiyo ya Marekani idara zake zinapaswa kusitisha biashara zote zinazoendesha mtandao huo wa kigaidi na kudhibiti usafirishaji wa fedha ndani ya makundi hayo.
Pamoja na kundi hilo kuwepo zaidi nchini Nigeria lakini Marekani inasema limekuwa likishirikiana na mtandao wa kimataifa wa Ugaidi wa Al Qaeda ambapo matawi yake yapo pia Afrika Magharibi na Mali.
Kundi hili la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2009 huku mashambulizi yake yakielekezwa katika vituo vya jeshi,katika shule na kuendesha mapigano na vikosi vya ulinzi nchini Nigeria.
Wachambuzi wa masuala ya kigaidi wanasema kuwa tamko hilo haliwezi kuwa mwarubaini wa kulinyong’onyeza kundi hilo kifedha kwa sababu wao hawapo nchini Marekani na wamekuwa wakipata fedha kwa kupitia njia ya kuteka nyara.
REUTERS
Mwisho.

300 wahofiwa kufariki Somalia

MOGADISHU, Somalia
WATU 300 wanahofiwa kufariki dunia katika eneo ya kaskazini mashariki mwa Somalia la Putland kutokana na kimbunga kikali na mvua kubwa iliyonyesha katika siku kadhaa kwenye eneo hilo.
Serikali ya Somalia imetangaza kuwa mvua kubwa, kimbunga kikali na mafuriko vimesababisha hali ya hatari na kwamba watu 300 wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha na mamia hawajulikani waliko.
Japokuwa takwimu hizo hazijathibitishwa na chombo cha kujitegemea lakini wataalamu wa masuala ya hewa wa Shirika la Chakula la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wanasema kuwa, mafuriko yalikuwa makubwa katika maeneo hayo ya kaskazini mashariki mwa Somalia.
Majuzi Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Puntland Abdirahman Mohamud Farole aliiomba jamii ya kimataifa kutuma misaada ya dharura kwa watu walioathika wa eneo hilo.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text