Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, November 3, 2013



Wanahabari wawili wa RFI wauawa Mali

BAMAKO, Mali
WAANDISHI wa habari wawili wa Redio France International (RFI) wameuawa siku juzi muda mfupi baada ya kutekwa na watu waliojihami kwa silaha kaskazini mwa nchini hapa.
Wanahabari hao waliotambuliwa kwa jina la Ghislane Dupont na Claude Verlon wameuawa muda mfupi baada ya kumaliza mahojiano yao na msemaji wa kundi la MNLA, Ambery Ag Rissa.
Kwa mujibu wa Ag Rissa, waandishi hao walikamatwa mbele ya nyumba yake na watu wasiofahamika na aligundua baada ya kusikia kelele lakini alipojaribu kutoka nje alitishiwa na kutakiwa kubaki kimya kisha gari la watekaji kuondoka na wanahabari hao ambao baadaye walionekana wakiwa wameuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Tinessako nje kidogo ya mji wa Kidal.
Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imethibitisha vifo hivyo na Rais Francois Hollande ameitisha mkutano wa dharura wa mawaziri kuzungumzia suala hilo.
Bado haijafamika chanzo cha mauaji hayo ingawa kikao cha dharura kinatarajiwa kuzungumzia iwapo tukio hilo lina uhusiano na hatua ya Ufaransa kupeleka majeshi yao kupambana na makundi ya wapiganaji huko Kaskazini mwa Mali tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Tayari Rais Hollande amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita kuhusiana na tukio hilo ambali limekuja siku chache baada ya raia wanne wa Ufaransa waliokuwa wakishikiliwa kama mateka nchini Niger tangu mwaka 2010 kuachiwa huru na kurejea nchini mwao.
Ghislane Dupont alifariki akiwa na miaka 57, enzi za uhai wake alikuwa mwanahabari wa kike akiandika zaidi habari za Afrika tangu alipojiunga na RFI mwaka 1986, amesharipoti habari katika mataifa ya Ethiopia, Sudan kwa miaka 10 akiwa mwakilishi wa RFI nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
RFI imesema Claude Verlon (55) alijiunga nao tangu mwaka 1982 na alikuwa akitumika kwa baadhi ya nyakati kuripoti matukio toka katika maeneo yenye migogoro duniani.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text