Biden: China, Marekani tanueni ushirikiano
HONGKONG, China
MAKAMU wa
Rais wa Marekani, Joe Biden, amezitaka China na Marekani ziimarishe na kutanua ushirikiano
kwa kivitendo wenye kuonesha matokeo chanya.
![]() |
| biden akikagua gwaride nchini China |
Pamoja na
kusisitiza kutanuka kwa ushirikiano lakini alikosoa mfumo wa elimu na utawala unaotumiwa
na nchi ya China.
Ziara ya
Biden iliyokuwa ya ghafla katika ubalozi wa Marekani nchini China, ilikuwa na
madhumuni ya kutafuta uungwaji mkono wa mpango wa Marekani wa kupunguza vikwazo
kwa Wachina wanaotaka kuingia Marekani.
Biden
ameliambia kundi la watu hao ambao wengi ni vijana, kwamba anatarajia wakati wa
kutembelea Marekani umefika ambako watapata fursa ya kujifunza kwamba uvumbuzi
unakuja pindi mtu anapopumua kwa uhuru.
"Nchini
Marekani, watoto wanazawadiwa kwa kuupa changamoto mfumo uliopo na sio
kuadhibiwa, na njia pekee ya kupata kipya ni kuondoa cha zamani." Biden
aliwaambia vijana hao.
Kauli kama
hii inayouokosoa mfumo wa utawala na kielimu wa China iliwahi kuzua mzozo baina
ya nchi hizo mbili Mei mwaka huu, baada ya Biden kuwaeleza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Pennsylvania kwamba huwezi kufikiri tofauti katika taifa ambalo huwezi kuvuta
hewa kwa uhuru, kauli iliyowaudhi wanafunzi wa chuo hicho na kusema wametukanwa
na hivyo kuomba waombwe radhi.
Katika ziara
yake Biden alipata wasaa wa kukutana na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao,
kwenye jengo la Ukumbi wa Watu wa China, ambapo alisifia jitihada za Rais Xi
katika kutatua tofauti zilizopo baina ya Marekani na China.

0 comments:
Post a Comment