Obama avionya vikosi vya uasi Sudani
Kusini
JUBA, Sudan
Kusini
RAIS wa
Marekani Barack Obama juzi amevionya vikosi vya waasi nchini Sudan Kusini vinavyofanya
mapinduzi ya kijeshi baada ya kuwajeruhi wanajeshi wanne wa Marekani.
Hayo
yamebainishwa kwenye taarifa kutoka ya Ikulu ya nchi hiyo imeeleza kuwa juhudi
zozote za kunyakua madaraka kwa nguvu za kijeshi zitakazosababisha kukoma kwa
msaada wa muda mrefu kutoka Marekani na Jumuiya ya kimataifa.
Rais Obama
amesisitiza kuwa viongozi wa Sudan Kusini wanalo jukumu la kusaidia juhudi za
Marekani kuwaokoa wamarekani na raia wengine huko Juba na Bor mji ambao
unashikiliwa na waasi.
Onyo la rais
Obama linatolewa baada ya ndege tatu za Marekani kushambuliwa kwa risasi wakati
zikielekea Bor kusaidia juhudi za kuwaondoa Wamarekani nchini Sudani Kusini kutokana
na kuchachamaa kwa mapigano baina ya serikali na waasi.
Jeshi la Serikali
ya Sudan Kusini lipo kwenye harakati za kutaka kuukomboa mji wa Bor, ulioko kaskazini
mwa mji mkuu Juba, kutoka wanajeshi walioasi na kumuunga mkono makamu wa rais
wa zamani, Riek Machar aliyefukuzwa kazi hivi karibuni na rais wa nchini humo, Silva
Kiir.
Baada ya kutangazwa
kutekwa kwa mji huo mara moja, Marekani ilipeleka wanajeshi wake 45 kuwalinda
raia wake wanaofanyashughuli zao hapo na mali zao.
Kuna taarifa
zinasema kuwa ndege za Uganda pia zimekuwa zikihusika katika kusaidia serikali ya
Sudan kuukomboa mji wa Bor kutoka kwa wanajeshi walioasi.
Wakati hayo
yakijili kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar amesema kuwa, vikosi
vyake vimefanikiwa kuchukua udhibiti wa jimbo muhimu la uzalishaji mafuta la
Unity nchini humo.
Makamu huyo
wa zamani wa rais amedai kuwa, vikosi vyake ambavyo vinapambana na askari wa
serikali vinadhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo. Kabla ya hapo pia jeshi la
Sudan Kusini lilikuwa limetangaza habari ya kujiengua serikalini kwa Jenerali
James Kwang Chol aliyekuwa kiongozi wa kijeshi katika jimbo hilo la Unity
nchini humo na kujiunga na waasi.
Habari
kutoka Addis Ababa, Ethiopia zinasema kuwa, ripoti iliyotolewa na Umoja wa
Mataifa zinasema kuwa AU imelaani vikali mauaji dhidi ya askari wa kulinda
amani wa UN na raia wasio na hatia, yaliyotekelezwa katika kambi ya nchini hapa.
Mapigano
hayo yalizuka siku ya Jumapili iliyopita mjini Juba, ambao ni mji mkuu wa Sudan
Kusini na hatimaye kuenea katika maeneo mengine ya nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment