Chama tawala
cha Gabon chashinda uchaguzi wa majimbo
LIBREVILLE, Gabon
CHAMA tawala
cha Democratic(PDG), ambacho kimeongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka 45, kimeshinda
kwenye uchaguzi wa majimbo uliofanyika Desemba 14.
Akitangaza
matokeo rasmi ya uchaguzi huo juzi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Gabon Jean
Francois Ndongou amesema Madiwani 1,500 kati ya 2,404 wa Chama cha PDG
wameshinda kwenye uchaguzi huo.
Chama hicho
kimechukua majimbo 122, lakini kimepoteza majimbo ya Mouila, Bakoumba Oyem na
Mitzic.
Matokeo hayo
yanaweza kurekebishwa au kutenguliwa na mahakama ya katiba, ambayo ina uwezo wa
kushughulikia mizozo ya uchaguzi.
Juzi
asubuhi, Waziri Mkuu wa zamani Jean Eyeghe Ndong, ambaye chama chake cha
Libreville kimechukua nafasi ya tatu, alisema yupo tayari kwa mazungumzo na
chama tawala ili kuunda serikali ya muungano.
0 comments:
Post a Comment